Share
Idadi ya vijana hapa nchini wanaendelea kulalamikia ukosefu wa ajira. Idadi ya vijana hapa nchini ikiwa ni milioni 13,777,600. Hii ikiwa ni asilimia 29 ya idadi ya watu hapa nchini Kenya.
Katika data ya sensa ya mwaka wa 2019 ikionyesha kuwa ni asilimia 38.9 ya Vijana ambao hawana kazi,hii ni sawia na zaidi ya milioni tano ya wanaotafuta ajira.
Katika mtaa wa gatina ulio na nafasi ya 1.5 Kilo mita kwa mraba na wenyeji Zaidi ya elfu arubaini ,linus Gitanga ambaye ana umri wa miaka ishirini na sita,na kuwa nataaluma ya upishi ni miongoni mwa asilimia ya 38.9 ya vijana waliokosa kazi katika kaunti ndogo ya Dagoretti. Gitanga ananidokezea kwa takribani miezi sita akiwa amesalia nyumbani kwa kukosa ajira.
“ Tangu uchaguzu utamatike nimekuwa mwathiria wa kukosa kazi. Nilikuwa nimeajiriwa kwenye sehemu ya burundani mtaa wa kileleshwa ila kazi yangu ilitamatika tuu baada ya gavana wa kaunti ya Nairobi kuapishwa na kuagiza vyumba vya burundani katika maeneo ya kuishi yakufungwa. Kila mara nikitembea kutafuta naambiwa watu ni wengi. Nazidi kusubiria tuu,” Gitanga.
Kwa upande wake jane ambaye ni mama wa watoto wanne anasema kuwa kufadhili masomo na kupata chakula imekuwa ngumu , “mimi ni mkaazi wa Kawangware, tangu tufanye uchanguzi hali kwangu imekuwa ngumu. Masomo imekuwa ngumu, chakula kupata ni ngumu na biashara ni ngumu kwa kuwa hakuna pesa.”
Kilo mita nne, natumia pikipiki kuelekea wadi ya kabiro ambayo ina nafasi ya 1.2 Kilo mita kwa mraba ,sehemu hii ikiwastili wakaazi elfu thelethini na nne. Hapa nakutana naye na mfanyabiashara na vile msanii steve mnyenge. Mnyenge analalamikia hali kuwa ngumu na kutaka viongozi waliopo mamlakani kuhakisha kuna maelewano ili sekta ya usanii na biashara imeinuka. Mnyenge ni miongoni mwa wale waliofungu biashara wakati wa maandamano katika mtaa huo. “unavyo niona hivi naishi kwa nyumba ya elfu tano na hii ya biashara nalipia shilingi elfu nne. Nikiweka hizi pesa kwa pamoja ni silingi elfu 9. Unaona wakati wa maandamano ilinilazimu nifunge kwa kuwa ukiwacha biashara wazi, hawa watu watakuja kula bila kulipia na mafuta na unga nimekopa,” asema Mnyenge.
Mwenyekiti wa bunge la mwananchi na vile mhubiri Wilson Thomas anasikitika kwa kuwa vijana wengi walikuwa na tumaini ya kupata kazi baada ya uchanguzi. Thomas amekashifu jinsi wanasiasa wanaozidi kuwapa vijana tumaini ya kazi kwa kuwa wakati wa maandamano vijana wamekuwa wakijikita mtaa huo na kufanya madhara.
Katibu wa shirika la Amani katika kaunti ndogo ya Dagoretti Omar Elkana anasema kuwa wamekuwa wakipokea ripoti jinsi vijana wanauliwa kiholela katika wadi ya Gatina na Kabiro kutokana na ukosefu wa kazi. Omar anawataka washika dau kufanya mikutano ya kuhakikisha kuwa amani inaendelezwa na swala la mauaji yanatamatishwa.
Mwakilishi wa gatina kennedy swaka hata hivyo amewataka vijana kuwa wavumilivu huku serikali ikijiandaa kutenga pesa za bajeti yam waka wa 2023/2024 akitaja kuwa kunalotumaini la kuwapeleka vijana wa wadi yake katika shule za kiufundi na kuwaunganisha na mashirika yatakayowafadhili na mikopo ya kuendeleza biashara. “ kaunti ya Nairobi ilichapisha nafasi ya kazi na ninafahamu kila wadu itapata nafasi. Kwa saa hii kuna wale nimepeleka mafunzo ya kuendesha gari,” swaka.
Makala Haya Yamechapishwa na Mtaani Rdaio Kwa Ushirikiano Na Code For Africa, Kenya Community Media Network Na Baraza La Vyombo Vya Habari Katoliki (Cameco) Kupitia Msaada Kutoka Ushirikiano Wa Ujerumani Kama Sehemu Ya Mradi Wa Jukumu Letu La Kaunti Yetu.