Share
By Brian Muriithi
Serikali ya kaunti ya Kajaido inaendelea kuwekeza katika sekta ya afya kwa ushirkiano na washikadau kadhaa.
Mikakati iliyowekwa na kaunti imeplekea kujenga kwa hospitali katika wadi mbali mbali kama njia moja ya kuboresha huduma kwa wakaazi.
Kulingana na ripoti ya CDIP, Kajiado ina hospitali nne za kaunti ndogo, vituo kumi na saba vya afya na zahanati sabini na nane zinazosimamiwa na serikali ya kaunti.
Hata hivyo, hospitali zingine, vituo vya afya na zahanati zote ni mia moja hamsini na nne, zinazoendeshwa na mashirika ya kibinafsi, kidini, kijamii na yasiyo ya serikali. Vile vile hosipitali za kibinafsi zinaongoza kwa idadi ya vitanada zikifuata na hosipitali za umma.
Mbali na hayo, uwiano wa idadi ya madaktari kwa wagonjwa bila shaka ni ya kutia wasiwasi kwa vile daktari mmoja anafaa kuhudumia karibia wagonjwa elfu ishirini na saba huku uwiano wa idadi ya wauguzi kwa wagonjwa ni muuguzi mmoja kuhudumia wagonjwa karibia elfu moja na mia moja.
Isitoshe, wastani wa umbali wa kwenda kituo cha afya ni kilomita kumi na nne nukta tatu huku asilimia tisa nukta tisa tu ya watu wakiwa umbali wa chini ya kilomita, hadi kituo cha afya.
Kwengineko, katika kaunti ya Kajiado, magonjwa mbalimbali yanayosababisha maradhi yanauzoefu wa kutendeka mara kwa mara na kuenea zaidi baina ya watu. Magonjwa haya ni kama mfumo wa kupumua, kuhara, nimonia na maambukizi ya njia ya mkojo.
Kulingana na utafiti uliofanywa na KDHS mwaka wa elfu mbili na kumi na nne ni kwamba kaunti ya Kajiado imerekodi uelewa wa juu kuhusu ugonjwa wa Virusi Vya UKIMWI (VVU) kwa asilimia tisini na tisa nukta tatu ya wanawake na asilimia mia ya wanaume waliripoti ufahamu.
Kiwango cha maambukizi ya VVU katika kaunti ya Kajiado ni asilimia tatu nukta tisa ikilinganishwa na kiwango cha kitaifa cha asilimia 6.
Image: Hospitali ya kaunti ya Kajiado. Asili: KBS
Makala Haya Yamechapishwa na Domus Marie Fm Kwa Ushirikiano Na Code For Africa, Kenya Community Media Network Na Baraza La Vyombo Vya Habari Katoliki (Cameco) Kupitia Msaada Kutoka Ushirikiano Wa Ujerumani Kama Sehemu Ya Mradi Wa Jukumu Letu La Kaunti Yetu.