Share
By David Gikaria
Visa vya maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi vimeonekana kupanda maradufu katika kaunti ya Taita Taveta ikilinganishwa na visa vilivyoripotiwa katika mwaka 2020.
Mratibu wa kaunti hii kuhusu maswala ya ukimwi na magonjwa ya zinaa Charity Mwabili amedokeza kwamba kwa sasa visa 8,875 vya maambukizi ya ugonjwa huo vimeripotiwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, miongoni mwa visa hivi 5,414 ikiwa ni vijana walio chini ya umri wa miaka 15.
Haya yanajiri ikizingatiwa kuwa miaka ya hapo awali visa vya Ukimwi miongoni mwa watu kati ya umri was miaka 15 hadi 49 vilipungua. Haya ni kulingana na ripoti ya CDIP ya Taita Taveta.
Bi Mwabili amesisitiza kwamba wizara ya afya katika kaunti hii kwa ushirikiano na washikadau mbalimbali nchini wanapanga mikakati ya kuwahamasisha vijana kuhusu ukimwi na magonjwa ya zinaa,ikizingatiwa kwamba visa vingi vinavyochipuka vya maambukizi vinawaathiri vijana, hasa kutokana na kutokuwepo kwa miundo mbinu kabambe ya kuwapa vijana elimu ya jamii kuhusu jinsi ya kudhibiti msambao wa ugonjwa huu.
Licha ya hayo, washikadau wamesisitiza kuwa kuna haja ya kutumia kinga kama njia moja kudhiti ugijwa huu hatari.
Kutumia kinga wakati wa kujamiiana, matumizi salama ya sindano (ikiwa ni pamoja na watu katika kazi fulani, kama wauguzi na wachora ngozi (tattoo)) na kutambuliwa mapema ni hatua zinazosaidia kuzuia maambukizi ya Ukimwi na kuzuia kusambaza virusi kwa watu wengine.
Image: Ujumbe kuhusu ugonjwa wa Ukimwi. Asili: Volunteer Mission
Makala Haya Yamechapishwa na Mwanedu Fm Kwa Ushirikiano Na Code For Africa, Kenya Community Media Network Na Baraza La Vyombo Vya Habari Katoliki (Cameco) Kupitia Msaada Kutoka Ushirikiano Wa Ujerumani Kama Sehemu Ya Mradi Wa Jukumu Letu La Kaunti Yetu.