Share
By Selestine Lunani
Wakaazi wa wadi ya Kaloleni eneo bunge la Voi kaunti ya Taita Taveta wametoa lawama kwa serikali ya kaunti kwa madai ya bajeti ya shilingi milioni 2.7 iliyotumiwa kwa ujenzi wa daraja la Kaloleni ,huku wakitaka serikali ya kaunti kufichua ukweli wa budgeti hiyo.
Kutokana na serikali kutoweka wazi bajeti ya muradi huo, wakaazi hawa wanatashwishwi ya kiwango hicho cha pesa kilichotumika kutokana na daraja hilo kuanza kuonyesha mianya ya kupasaka.
Haya yanajiri huku changamoto ikiendelea kutolewa kwa serikali ya kaunti ya Taita Taveta kuhakikisha inapanua daraja la kuvuka mto wa Voi kutoka Kasarani kuelekea mji wa Voi ili kurahisisha zaidi usafiri wa wananchi wanapotaka kutafuta huduma mbalimbali ikiwamo za matibabu katika hosipitali ya rufaa ya Moi,sawa na usafirishaji wa bidhaa zao za shambani.
Wakazi wa eneo la Kasarani hasusani wale ambao wanajihusisha na kilimo wakiongozwa na Dora Maghuwa wanasema japo daraja hilo liliweza kujengwa linastahili kupanuliwa ili kuruhusu uchukuzi ikiwamo wa bodaboda ili kuwawezesha wananchi kuafikia huduma wanazohitaji kwa wakati mwafaka
Bi Maghuwa pia ameelezea kuwa daraja hilo halikujengwa kwa njia inayostahili kwa kile anasema linatiwa wasiwasi wakati mtu anapovuka
Kadhalika wamepongeza ujenzi wa daraja hilo wakisema umewasaidia katika kuendeleza biashara zao kutokana na mazao ya shambani sawa na shughuli zingine za kila siku Wakati huo wanasema umesaidia wanafunzi wa shule kufika shuleni kwa wakati.
Aidha, lalama za wakaazi hao kuhusu kupanuliwa kwa daraja hilo kunajiri baada ya aliyekuwa waziri wa fedha na mipango katika serikali Leonard Langat kuelezea kupanuliwa kwa daraja hilo miaka mbili iliyopita ahadi ambayo hadi sasa haijatimizwa.
Haya yanajiri huku Kaunti ya Taita Taveta ikikadiria kuongezeka kwa ishara ya matokea katika sekta ya uchukuzi.
Kwa upande wake gavana Graton Samboja uwepo wa daraja hii umesaidia sana wenyeji wa wardi ya kaloleni hasa wafanyi biashara na wakulima.
Image: Kaloleni footbridge. Source: Department of Public Works & Infrastructure -Taita Taveta County
Makala haya yameandaliwa na Mwanedu FM kwa kushirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network (KCOMNET) na Baraza la vyombo vya habari katoliki (CAMECO) kupitia msaada wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa kaunti yetu , jukumu letu.