Share
By Joan Njeru
Baada ya rais Uhuru Kenyatta kuingia kwa mamlaka mwaka wa 2013, alileta wazo la kufufua upya shule za kutoa mafunzo ya kiufundi maarufu TVET, zilizokuwa zimefifia.
Shule hizi ziliazishwa na rais wa kwanza wa jamhuri ya Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta kwa nia ya kuhakikisha kuwa vijana wamepata mafunzo ya kazi za mikono kama njia mojawapo ya kuongeza ajira nchini.
Kuanzia mwaka wa 2013, vyuo vya TVET nchini vimeongezeka kwa 190% kutoka 753 hadi 2,191 mwaka wa 2019. Hii ni inashiria kuwa mikakati iliyowekwa na serikali iko na matokeo.
Baada ya mtihani wa kitaifa wa KCSE 2020, vyuo vya TVET vina uwezo wa kuhudumia wanafunzi 600,000. Muonekano mpya wa TVET nchini ulichangia pakubwa wanafunzi 4,840 waliohitimu alama zaidi ya C+ kuchagua kujiunga na vyuo hivi vya kiufundi. Lengo kuu la serikali ni kuhakisha kuwa wanafunzi waliokosa kujiunga na vyuo vikuu wanzaweza endeleza masomo.
Kuongezeka kwa shule za TVET ni matokeo ya mradi ulioanzishwa mwaka wa 2016. Rais Uhuru aliamrisha wizara ya elimu kuhakikisha kuwa kila eneo bunge limepata angalau chuo kimoja.
Vile vile, serikali za kaunti zinaendeleza mikakati ya kujenga na kukuza vyuo vya TVET. Kwa mfano, kaunti ya Kajiado ilikadiria kutenga shilingi milioni 283 kujenga vyuo vya TVET.
Kutokana na dhana potovu ya kuwa vyuo vya TVET ni vya wale waliofeli. Wanafunzi hasaa waliomaliza masomo yao ya shule ya upili,wanahimizwa kukumbatia mafunzo haya ya kiufundi.
Cha kutia moyo ni kuwa serikali ya Kenya inafadhili wanafunzi ambao wameweza kujisajilisha kusomea vyuo vya TVET.
Hatua ya serikali ya kuimarisha mtaala mpya wa elimu nchini CBC, inampa mwanafunzi nafsi ya kusomea somo ambalo amekuwa na hamu nalo, kwa hivyo kuweza kubobea katika taaluma fulani. Ni jambo ambalo litaboresha mafunzo ya ufundi wa mikono.Vile vile TVET ni chanzo cha kutia makali ufundi ambao mwanafunzi anao.
Image: TVET students. Source: Tuko
Makala haya yameandaliwa na Chumba cha Habari cha Bus Radio Ushirikiano na Code for Africa, Kenya Community Media Network na Baraza la Vyombo vya Habari Katoliki kwa msaada kutoka Ushirikiano wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa Kaunti Yetu, Jukumu Letu.